(Mount Kenya University, 2015-10) Muhidin, Zahor Mwalim
Wazanzibari hupenda kuchanganya lugha. Mara nyingi, wao huchanganya lugha ya Kiswahili,
Kiingereza na Kiarabu. Mtindo huu unaweza kuthibitishwa kihistoria kutokana na athari ya
mchanganyiko wa Waswahili wa Zanzibar na wageni wa Kiarabu kabla, wakati na baada ya
ukoloni; pamoja na majilio ya wageni wa kizungu wakati na baada ya ukoloni (Broomfield,.
1931; Krapf, 1878; na Topan, 1992).