Kiswahili and other African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Kiswahili and other African Languages by Author "Ireri, John Muriuki"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Publication Open Access Utathmini wa Maudhui katika Nyimbo Teule za Newton Kariuki(Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 2023-09-09) Ireri, John Muriuki; Ntiba, OnesmusMakala hii inahusu utathmini wa maudhui katika nyimbo teule za msanii Newton Kariuki. Nyimbo ni moja wapo ya njia zinazotumiwa na wasanii kuwaslisha ujumbe unaowahusu jamii. Utafiti huu ulitumia nadharia ya mseto, yaani nadharia ya umtindo ile ya udenguzi. Nadharia ya umtindo inasisitiza kuwa lugha ina sehemu mbili zinazodhihirika katika usemaji; lugha ni dhahiri na dhahania. Aidha, nadharia ya udenguzi huashiria mgogoro usiosuluhika uliopa baina ya usemi balagha na mawazo kwamba kuna pengo kati ya inachokusudia kusema kazi ya fasihi na inacholazimika au kuelekezwa kusema. Hivyo kuna mvuto katika ya usemi na mantiki. Utafiti ulichukua muundo wa kimaelezo. Mtafiti aliteua kimakusudi jumla ya nyimbo kumi zilizoimbwa na mwanamuziki Newton Kariuki, yaani tano za Kiswahili na tano za Kimbeere. Kutokana na jumla ya nyimbo hamsini alizokuwa ameimba kufikia muda wa kufanya utafiti. Data ilikusanywa kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Waaidha, data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo ya utafiti ni kuwa sampuli iliyoteuliwa ilisheheni maudhui ya mapenzi, ndoa na familia, migogoro katika ndoa, kuporomoka kwa maadili, uongozi na siasa, umaskini, uhalifu, mawaidha, UKIMWI na dini na imani. Maudhui haya yaliakisi maisha katika ulimwengu wa kiuhalisia. Umuhimu wa makala hii ni kuwa matokeo haya yanadhihirisha kuwa mwimbaji yeyote halengi tu kuburudisha bali kuelimisha. Hivyo makala hii inapendekeza utafiti wa baadae ufanywe kwa kuzingatia mahusiano ya uwezo wa kiuana katika sampuli teule.