Kiswahili and other African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Kiswahili and other African Languages by Title
Now showing 1 - 4 of 4
Results Per Page
Sort Options
Publication Open Access Athari za Udhanaishi wa Kidini kwa Vijana Katika Riwayaza Paradiso na Kidagaa Kimemwozea(International Journal of Social Science and Humanity Research, 2024-05) Murimi, Jackline Njeri; Muli, SolomonSuala la imani katika Mungu ni nyeti na linatiliwa maanani na binadamu katika tamaduni mbalimbali kote duniani kama njia mojawapo ya kujaribu kutafuta majibu ya changamoto anazokubana nazo kila uchao. Katika jamii nyingi za kiafrika,dini ni mfumo wa maisha (Mbithi 2011 )ambapo kila mwana jamii alihitajika kushiriki. Hata hivyo, suala hili la kidini linaonekana kuwatamausha vijana wengi na kufifisha imani yao katika dini. Hivyo ,utafiti h uu ulinuia kuchanganua baadhi ya athari za udhanaishi wa dini kwa vijana kwa kurejelea riwaya ya Paradiso na Kidagaa Kimemwozea zilizoandikwa na John Habwe na Ken Walibora m tawalia kwa ku chunguza jinsi John Habwe na K en Walibora wanavyoangazia udhanaishi wa kidini katika jamii . Katika kulizamia suala hili makala hii i liongoz w a na nadharia ya udhanaishi iliyoasisiwa na Mwanathiolojia kutoka Denmaki(1813 - 1855),Fredrick Nietzsche,Martin Heidegger,Gabriel Marcel na Karl Jaspers waliotokea karne ya 20 na Jean Paul Satre Mfaransa aliyetokea baada ya vita vya pili vya d unia. Mihimili yake ilisaidia kufikia malengo ya yetu . Mihimili mikuu ya nadh aria ya udhanaishi ni pamoja na ;kutilia mkazo matatizo halisi yanayomsibu mwanad amu na kuwa na imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi, inapalilia kutokuwepo kwa mungu na uumbaji wake wa ulimwengu,inatilia mkazo kuwa juhudi za mtu kujisaka au kujaribu kupambana na maisha huishia katika mauti, maudhui yake ni kama vile uhuru wa mtu bin afsi kuweza kufikiri halafu kutoa jawabu lake. Nadharia husimulia taabu na kuchoka na hali ambazo husumbua yanayotatiza mwana wa adamu, nadharia hii inajadili mkengeuko,nadharia hii inachora taswira ya mateso anayopitia mwanadamu duniani, nadharia hii in atilia mkazo kuwa maisha yamejawa na utupu na kihoro hasa kuhusu siku za kesho.Maisha yamejawa na ubwege na huhakikisha binadamu kuwa mwisho wa maisha ni kifo.Nadharia hii ilifaa utafiti kwani ilitumika kueleza jinsi baadhi ya vijana waumini wavavyoyaona m aisha jambo ambalo linawafanya watamaushwe na dini kila uchao. Nadharia hii ilitumika kupambanua ukweli wa je ni lipi ambalo baadhi ya vijana katika jamii wamejua hivi karibuni ambalo mababu zao hawakufahamu hapo awali?Utafiti ulifanyika maktabani kuliko n a vitabu, majarida,matini na magazeti na wa mtandaoni ambapo data ilipatikana kutokana na tasnifu zilizoandikwa kuhusu mkengeuko wa imani za kidini.Sampuli ya kimaksudi ilitumika katika kuteua riwaya ya Paradisona Kidagaa Kimemwozea . Mbinu anuwai za kima elezo zilitumika katika kuchambua data na kuiwasilisha kwa l ugha ya nadhari kuambatana na lengo l a utafiti. Maarifa yaliyopatikana katika utafiti huu yatakuwa na mchango mkubwa katika maarifa yaliyopo kuhusu vijana na masuala ya dini katika jamii.Publication Open Access Images of women in Agikuyu Mwomboko poetry: a selection from performing artists from Mount Kenya region(The Journal of Literature and Performing Arts, 2024-03-01) Mwangi, Peter MuhoroThe position of women in African societies has been contested in terms of their treatment in social and poetic discourse in contemporary society. The case of traditional and modern poetic dances is spelt out in the composing and rendition of Mwomboko poetry of the Agikuyu people of Mount Kenya Region. The objectives of this study are: (a) To assess how select compositions of Mwomboko poetry spell out treatment of women in Mount Kenya region community; (b) To analyze how figurative language is applied in select compositions of Mwomboko poetry to approximate images of women in Mount Kenya region community, and (c) To explore the innovativeness of oral poets’ poetic architecture in charting out the position of women in contemporary society. Popular artists in Africa have tended to be the mouth pieces of revealing the societal structures that spell out the relationship between men and women as shown through poetic discourse. The place of performance has emerged as a central pivot for linking up members of the community in their efforts to understand their worldview. The emergence of modern performers has created a new forum for capturing the imagination of target recipients in an open multi– ethnic audience. The audience has been mainly in hotels, motels and bars, social halls, wedding reception halls/grounds, political rally grounds, and church service halls among others. The current work hinges on the level of deconstruction theory as seen through feminist and gender lens in contemporary times. The images of women revealed in Mwomboko poetry are constructions by architects of the traditional cum modern poetic genre, and the findings reveal a move towards balanced portrayal of both genders in emergent renditions. The study uses descriptive techniques in analysis of figurative language applied by traditional and modern singers to approximate old meanings to new meanings in their performances as far as images of women are represented.Publication Open Access Usawiri wa waandishi wa jinsia tofauti wanavyoangazia Ukandamizaji wa kijamii katika riwaya za Maisha kitendawili Na Chozi la heri(Journal of Educational Research, 2024-01) Njeri, Jackline Murimi; Nkoroi, Maingi NancyKatika utafiti huu tumehakiki jinsi waandishi wa kiume na kike wanavyoangazia ukandamizaji wa kijinsia katika jamii kwa kurejelea riwaya za Chozi la Heri (Assumpta K. Matei) na Maisha Kitendawili (John Habwe). Utafiti huu unachunguza na kuchanganua kwa misingi ya kijinsia jinsi wahusika mbalimbali wanavyotengwa na kukandamizwa na jamii. Aidha, utafiti umechanganua jinsi waliotengwa na kukandamizwa na jamii wanavyosawiriwa katika macho ya waandishi wa kiume na wa kike. Isitoshe mapendekezo ya utatuzi wa matatizo haya yamedokezwa kwa kurejelea waandishi John Habwe na Assumpta K. Matei. Imebainika kuwa John Habwe amesawiri jinsia ya kike kama jinsia inayokandamizwa zaidi mikononi mwa yule wa kiume tofauti na Assumpta Matei ambaye ameangazia jinsia ya kiume kama jinsia iliyo na matatizo mengi ikilinganishwa na ile ya kike. Utafiti huu, uliongozwa na nadharia ya Jinsia -Hakiki iliyoasisiwa na mfeministi Showalter Elaine katika mwaka wa 1840. Nadharia hii hutumiwa kuhakiki kazi zakifasihi zilizoandikwa na watunzi wa jinsia tofauti tofauti. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu mathalan utafitiwa maktabani ambapo tulisoma vitabu, majarida, matini na magazeti mbalimbali ili kukusanya data yetu. Pia tumesoma maandishi mbalimbali yanayolenga mada yetu hasa yale yaliyoandikwa na jinsia ya kiume na kike kuhusu ukandamizaji. Zaidi ya hayo, tumechakura mtandao ili kuweza kuelewa zaidi kuhusu kipengele cha ukandamizaji katika jamii. Tumetumia uteuzi wa sampuli wa kiamksudi katika kuteua riwaya ya Maisha Kitendawili na Chozi la Heri. Riwaya hizi mbili zimeandikwa na watunzi mwanamume na mwanamke ambao ni watunzi wa kazi za Kiswahili nchini Kenya. Tulikusanya data yetu kutoka kwa riwaya ya Maisha Kitendawili na Chozi la Heri.Aidha, tulipata data yetu kutoka mtandaoni, vitabuni, makala, maktabani na kwenye tasnifu. Tuliichanganua data yetu kwa kutumia maelezo na tarakimu,maelezo na ufafanuzi kuwasilisha data. Data hii ilitusaidia kutathmini kama waandishi wa jinsia ya kiume na kike wanaangazia masuala ya ukandamizaji kwa njia sawa ama kwa njia tofauti.Utafiti huu unanuiwa kunamfaa mwanafasihi katika kupata maarifa na uzoefu wa uhakiki kuhusu mwanajamii aliyetengwa na kuelewa kwa undani kazi mbalimbali zinazoangazia utetezi wa jinsia mbalimbali zilizotengwa katika jamii. Kazi hii vilevile inatusaidia katika kuangazia na kuweka wazi namna ambavyo waandishi wa kike na wa kiume wanavyochangia katika kushughulikia masuala ya ukandamizaji wa jinsia mbalimbali na mambo yanayohusu jamii tunamoishi. Isitoshe, utafiti huu unachangia katika kutoa suluhu ya namna mbalimbali za kushughulikia suala la kukandamizwa kwa jinsia mbalimbali.Publication Open Access Utathmini wa Maudhui katika Nyimbo Teule za Newton Kariuki(Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 2023-09-09) Ireri, John Muriuki; Ntiba, OnesmusMakala hii inahusu utathmini wa maudhui katika nyimbo teule za msanii Newton Kariuki. Nyimbo ni moja wapo ya njia zinazotumiwa na wasanii kuwaslisha ujumbe unaowahusu jamii. Utafiti huu ulitumia nadharia ya mseto, yaani nadharia ya umtindo ile ya udenguzi. Nadharia ya umtindo inasisitiza kuwa lugha ina sehemu mbili zinazodhihirika katika usemaji; lugha ni dhahiri na dhahania. Aidha, nadharia ya udenguzi huashiria mgogoro usiosuluhika uliopa baina ya usemi balagha na mawazo kwamba kuna pengo kati ya inachokusudia kusema kazi ya fasihi na inacholazimika au kuelekezwa kusema. Hivyo kuna mvuto katika ya usemi na mantiki. Utafiti ulichukua muundo wa kimaelezo. Mtafiti aliteua kimakusudi jumla ya nyimbo kumi zilizoimbwa na mwanamuziki Newton Kariuki, yaani tano za Kiswahili na tano za Kimbeere. Kutokana na jumla ya nyimbo hamsini alizokuwa ameimba kufikia muda wa kufanya utafiti. Data ilikusanywa kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Waaidha, data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo ya utafiti ni kuwa sampuli iliyoteuliwa ilisheheni maudhui ya mapenzi, ndoa na familia, migogoro katika ndoa, kuporomoka kwa maadili, uongozi na siasa, umaskini, uhalifu, mawaidha, UKIMWI na dini na imani. Maudhui haya yaliakisi maisha katika ulimwengu wa kiuhalisia. Umuhimu wa makala hii ni kuwa matokeo haya yanadhihirisha kuwa mwimbaji yeyote halengi tu kuburudisha bali kuelimisha. Hivyo makala hii inapendekeza utafiti wa baadae ufanywe kwa kuzingatia mahusiano ya uwezo wa kiuana katika sampuli teule.