Browsing by Author "Ntiba, Onesmus Gitonga"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Publication Open Access Ushawishi za nyimbo za kampuni wa jamii ya Wachuka katika kaunti ya Tharaka Nithi, Kenya(Mount Kenya University, 2016-11) Ntiba, Onesmus GitongaTasnifu hii inahusu uhakiki wa usemi wa nyimbo za kampeni za jamii ya Wachuka katika kaunti ya Tharaka Nithi. Nyimbo za kampeni ambazo tumezingatia ni zile zilizokuwa zinaimbwa kati ya 1992-2013. Wachuka ni mojawapo wa makundi ya Wameru wanaozungumza lahaja ya Kichuka. Katika utafiti huu, tumelenga kuangazia jinsi ushawishi wa kisiasa umejengwa kupitia vipashio mbalimbali vya lugha, ujumbe na mitindo anuwai katika nyimbo hizi. Kufanikisha shughuli hii, tumezingatia mtindo changamano unaojumlisha mihimili kutoka Nadharia ya Uchanganuzi Usemi Hakiki na Nadharia ya Umitindo. Data ambayo tumeshughulikia katika utafiti huu tuliipata nyanjani katika tarafa za Chuka, Magumoni na Igambang’ombe katika Kaunti ya Tharaka Nithi. Data hii tuliipata kupitia aina ya rununu iliyokuwa na uwezo wa kupiga picha na kunasa nyimbo tulizokuwa tunaimbiwa na wahojiwa. Kwanza, nyimbo hizi ziliandikwa kwa Kichuka kisha kutafsiriwa kwa Kiswahili.