Publication: Ushawishi za nyimbo za kampuni wa jamii ya Wachuka katika kaunti ya Tharaka Nithi, Kenya
Total Views 15
total viewsTotal Downloads 96
total downloadsDate
2016-11
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Mount Kenya University
Cite this Item
Abstract
Tasnifu hii inahusu uhakiki wa usemi wa nyimbo za kampeni za jamii ya Wachuka
katika kaunti ya Tharaka Nithi. Nyimbo za kampeni ambazo tumezingatia ni zile
zilizokuwa zinaimbwa kati ya 1992-2013. Wachuka ni mojawapo wa makundi ya
Wameru wanaozungumza lahaja ya Kichuka. Katika utafiti huu, tumelenga kuangazia
jinsi ushawishi wa kisiasa umejengwa kupitia vipashio mbalimbali vya lugha, ujumbe na
mitindo anuwai katika nyimbo hizi. Kufanikisha shughuli hii, tumezingatia mtindo
changamano unaojumlisha mihimili kutoka Nadharia ya Uchanganuzi Usemi Hakiki na
Nadharia ya Umitindo. Data ambayo tumeshughulikia katika utafiti huu tuliipata
nyanjani katika tarafa za Chuka, Magumoni na Igambang’ombe katika Kaunti ya Tharaka
Nithi. Data hii tuliipata kupitia aina ya rununu iliyokuwa na uwezo wa kupiga picha na
kunasa nyimbo tulizokuwa tunaimbiwa na wahojiwa. Kwanza, nyimbo hizi ziliandikwa
kwa Kichuka kisha kutafsiriwa kwa Kiswahili.
Description
Keywords
Tharaka , Nithi, Nyimbo za Kampeni