(Mount Kenya University, 2015-10) Nyangeri, Nahashon Akungah
Lugha ya Kiswahili inadhihirisha utajiri mkubwa ambao haujafumbatiwa na wanaisimu
kikamilifu. Utajiri wenyewe unadhihirika kutokana na wingi wa lahaja zake. Hii ina maana
kwamba ikiwa kutaandikwa kamusi kamilifu ya Kiswahili, itakuwa kanzi kubwa na toshelezi,
kinyume na kamusi zilizopo.