(Mount Kenya Univeristy, 2015-10) Wanjala, F. C. N. S.
Nadharia ya Mwingilianotanzu inashikilia kuwa, kazi yoyote ya fasihi simulizi hujengwa kwa
kuvunja mipaka ya kitanzu ili kuibuka na kazi mahuluti. Hii ina maana kuwa, hakuna kazi ya
fasihi simulizi ambayo inaweza kukamilika bila kuchanganyikana na kazi nyinginezo za
fasihi. Malengo makuu ya nadharia hii ni kupinga uchambuzi wa utanzu mmoja mmoja wa
fasihi simulizi kana kwamba upo utanzu unaoweza kujisimamia kiutendakazi bila kuingiliana
na tanzu zingine.