Kiswahili and other African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Kiswahili and other African Languages by Subject "Jinsia"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Publication Open Access Usawiri wa waandishi wa jinsia tofauti wanavyoangazia Ukandamizaji wa kijamii katika riwaya za Maisha kitendawili Na Chozi la heri(Journal of Educational Research, 2024-01) Njeri, Jackline Murimi; Nkoroi, Maingi NancyKatika utafiti huu tumehakiki jinsi waandishi wa kiume na kike wanavyoangazia ukandamizaji wa kijinsia katika jamii kwa kurejelea riwaya za Chozi la Heri (Assumpta K. Matei) na Maisha Kitendawili (John Habwe). Utafiti huu unachunguza na kuchanganua kwa misingi ya kijinsia jinsi wahusika mbalimbali wanavyotengwa na kukandamizwa na jamii. Aidha, utafiti umechanganua jinsi waliotengwa na kukandamizwa na jamii wanavyosawiriwa katika macho ya waandishi wa kiume na wa kike. Isitoshe mapendekezo ya utatuzi wa matatizo haya yamedokezwa kwa kurejelea waandishi John Habwe na Assumpta K. Matei. Imebainika kuwa John Habwe amesawiri jinsia ya kike kama jinsia inayokandamizwa zaidi mikononi mwa yule wa kiume tofauti na Assumpta Matei ambaye ameangazia jinsia ya kiume kama jinsia iliyo na matatizo mengi ikilinganishwa na ile ya kike. Utafiti huu, uliongozwa na nadharia ya Jinsia -Hakiki iliyoasisiwa na mfeministi Showalter Elaine katika mwaka wa 1840. Nadharia hii hutumiwa kuhakiki kazi zakifasihi zilizoandikwa na watunzi wa jinsia tofauti tofauti. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu mathalan utafitiwa maktabani ambapo tulisoma vitabu, majarida, matini na magazeti mbalimbali ili kukusanya data yetu. Pia tumesoma maandishi mbalimbali yanayolenga mada yetu hasa yale yaliyoandikwa na jinsia ya kiume na kike kuhusu ukandamizaji. Zaidi ya hayo, tumechakura mtandao ili kuweza kuelewa zaidi kuhusu kipengele cha ukandamizaji katika jamii. Tumetumia uteuzi wa sampuli wa kiamksudi katika kuteua riwaya ya Maisha Kitendawili na Chozi la Heri. Riwaya hizi mbili zimeandikwa na watunzi mwanamume na mwanamke ambao ni watunzi wa kazi za Kiswahili nchini Kenya. Tulikusanya data yetu kutoka kwa riwaya ya Maisha Kitendawili na Chozi la Heri.Aidha, tulipata data yetu kutoka mtandaoni, vitabuni, makala, maktabani na kwenye tasnifu. Tuliichanganua data yetu kwa kutumia maelezo na tarakimu,maelezo na ufafanuzi kuwasilisha data. Data hii ilitusaidia kutathmini kama waandishi wa jinsia ya kiume na kike wanaangazia masuala ya ukandamizaji kwa njia sawa ama kwa njia tofauti.Utafiti huu unanuiwa kunamfaa mwanafasihi katika kupata maarifa na uzoefu wa uhakiki kuhusu mwanajamii aliyetengwa na kuelewa kwa undani kazi mbalimbali zinazoangazia utetezi wa jinsia mbalimbali zilizotengwa katika jamii. Kazi hii vilevile inatusaidia katika kuangazia na kuweka wazi namna ambavyo waandishi wa kike na wa kiume wanavyochangia katika kushughulikia masuala ya ukandamizaji wa jinsia mbalimbali na mambo yanayohusu jamii tunamoishi. Isitoshe, utafiti huu unachangia katika kutoa suluhu ya namna mbalimbali za kushughulikia suala la kukandamizwa kwa jinsia mbalimbali.