Kiswahili and other African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Kiswahili and other African Languages by Subject "Ken Walibora"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Publication Open Access Athari za Udhanaishi wa Kidini kwa Vijana Katika Riwayaza Paradiso na Kidagaa Kimemwozea(International Journal of Social Science and Humanity Research, 2024-05) Murimi, Jackline Njeri; Muli, SolomonSuala la imani katika Mungu ni nyeti na linatiliwa maanani na binadamu katika tamaduni mbalimbali kote duniani kama njia mojawapo ya kujaribu kutafuta majibu ya changamoto anazokubana nazo kila uchao. Katika jamii nyingi za kiafrika,dini ni mfumo wa maisha (Mbithi 2011 )ambapo kila mwana jamii alihitajika kushiriki. Hata hivyo, suala hili la kidini linaonekana kuwatamausha vijana wengi na kufifisha imani yao katika dini. Hivyo ,utafiti h uu ulinuia kuchanganua baadhi ya athari za udhanaishi wa dini kwa vijana kwa kurejelea riwaya ya Paradiso na Kidagaa Kimemwozea zilizoandikwa na John Habwe na Ken Walibora m tawalia kwa ku chunguza jinsi John Habwe na K en Walibora wanavyoangazia udhanaishi wa kidini katika jamii . Katika kulizamia suala hili makala hii i liongoz w a na nadharia ya udhanaishi iliyoasisiwa na Mwanathiolojia kutoka Denmaki(1813 - 1855),Fredrick Nietzsche,Martin Heidegger,Gabriel Marcel na Karl Jaspers waliotokea karne ya 20 na Jean Paul Satre Mfaransa aliyetokea baada ya vita vya pili vya d unia. Mihimili yake ilisaidia kufikia malengo ya yetu . Mihimili mikuu ya nadh aria ya udhanaishi ni pamoja na ;kutilia mkazo matatizo halisi yanayomsibu mwanad amu na kuwa na imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi, inapalilia kutokuwepo kwa mungu na uumbaji wake wa ulimwengu,inatilia mkazo kuwa juhudi za mtu kujisaka au kujaribu kupambana na maisha huishia katika mauti, maudhui yake ni kama vile uhuru wa mtu bin afsi kuweza kufikiri halafu kutoa jawabu lake. Nadharia husimulia taabu na kuchoka na hali ambazo husumbua yanayotatiza mwana wa adamu, nadharia hii inajadili mkengeuko,nadharia hii inachora taswira ya mateso anayopitia mwanadamu duniani, nadharia hii in atilia mkazo kuwa maisha yamejawa na utupu na kihoro hasa kuhusu siku za kesho.Maisha yamejawa na ubwege na huhakikisha binadamu kuwa mwisho wa maisha ni kifo.Nadharia hii ilifaa utafiti kwani ilitumika kueleza jinsi baadhi ya vijana waumini wavavyoyaona m aisha jambo ambalo linawafanya watamaushwe na dini kila uchao. Nadharia hii ilitumika kupambanua ukweli wa je ni lipi ambalo baadhi ya vijana katika jamii wamejua hivi karibuni ambalo mababu zao hawakufahamu hapo awali?Utafiti ulifanyika maktabani kuliko n a vitabu, majarida,matini na magazeti na wa mtandaoni ambapo data ilipatikana kutokana na tasnifu zilizoandikwa kuhusu mkengeuko wa imani za kidini.Sampuli ya kimaksudi ilitumika katika kuteua riwaya ya Paradisona Kidagaa Kimemwozea . Mbinu anuwai za kima elezo zilitumika katika kuchambua data na kuiwasilisha kwa l ugha ya nadhari kuambatana na lengo l a utafiti. Maarifa yaliyopatikana katika utafiti huu yatakuwa na mchango mkubwa katika maarifa yaliyopo kuhusu vijana na masuala ya dini katika jamii.