Publication: Athari za udhanaishi wa kidini kwa vijana katika riwaya teule za paradiso na kidagaa kimemwozea
Total Views 6
total viewsTotal Downloads 85
total downloadsDate
2024-06
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Mount Kenya University
Cite this Item
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchanganua sababu zilizowafanya baadhi ya vijana katika jamii
kutamaushwa na dini kwa kurejelea riwaya ya John Habwe Paradiso(2005)na ya Ken Walibora
Kidagaa Kimemwozea(2012).Kwa mujibu wa Mbithi(2011),suala la imani katika Mungu ni
nyeti na linatiliwa maanani na binadamu katika tamaduni mbalimbali kote duniani kama njia
mojawapo ya kujaribu kutafuta majibu ya changamoto anazokubana nazo kila uchao.Katika
jamii nyingi za Kiafrika,dini ni mfumo wa maisha ambapo kila mwana jamii alihitajika
kushiriki.Hata hivyo,suala hili la kidini linaonekana kuwatamausha vijana wengi na kufifisha
imani
yao
katika
dini.
.
Mtafiti alichunguza jinsi John Habwe na Ken Walibora wanavyoangazia udhanaishi wa kidini
katika jamii.Ili Kukamilisha lengo hili kuu,malengo matatu mahususi yalizingatiwa.Malengo
hayo ni pamoja na:kujadili vichocheo vinavyofanya vijana kutamaushwa na dini kwa mujibu wa
riwaya teule za Paradiso na Kidagaa Kimemwozea,kutathmini athari zinazotokana na utamaushi
wa kidini kwa mujibu wa riwaya teule za Paradiso na kidagaa kimememwozea na kuchanganua
njia mbadala zinazoweza kutumiwa kuondoa utamaushi huu na kujenga imani ya umri wa vijana
katika dini.
Utafiti uliongoza na nadharia ya Udhanaishi iliyoasisiwa na Mwanathiolojia kutoka
Denmaki(1813-1855),Fredrick Nietzsche,Martin Heidegger,Gabriel Marcel na Karl Jaspers
waliotokea karne ya 20 na Jean Paul Satre Mfaransa aliyetokea baada ya vita vya pili vya
dunia.Mihimili yake ilisaidia mtafiti kufikia malengo ya utafiti. Mihimili mikuu ya nadharia ya
udhanaishi ni pamoja na ;kutilia mkazo matatizo halisi yanayomsibu mwanadamu na kuwa na
imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi,inapalilia kutokuwepo kwa mungu na uumbaji wake wa
ulimwengu,inatilia mkazo kuwa juhudi za mtu kujisaka au kujaribu kupambana na maisha
huishia katika mauti,maudhui yake ni kama vile uhuru wa mtu binafsi kuweza kufikiri halafu
kutoa jawabu lake.Nadharia husimulia taabu na kuchoka na hali ambazo husumbua yanayotatiza
mwana wa adamu,nadharia hii inajadili mkengeuko,nadharia hii inachora taswira ya mateso
anayopitia mwanadamu duniani,nadharia hii inatilia mkazo kuwa maisha yamejawa na utupu na
kihoro hasa kuhusu siku za kesho.Maisha yamejawa na ubwege na huhakikisha binadamu kuwa
mwisho wa maisha ni kifo.Nadharia hii ilifaa utafiti kwani ilitumika kueleza jinsi baadhi ya
vijana waumini wanavyofasiri maisha jambo ambalo linawafanya watamaushwe na dini kila
uchao.Nadharia hii ilitumika kupambanua ukweli wa je ni lipi ambalo baadhi ya vijana katika
jamii wamejua hivi karibuni ambalo mababu zao hawakufahamu hapo awali?Utafiti ulifanyika
maktabani kuliko na vitabu,majarida,matini na magazeti. Pia kulikuwa na shughuli za mtandaoni
ambapo data ilipatikana kutokana na tasnifu zilizoandikwa kuhusu mkengeuko wa imani za
kidini.Sampuli ya kimaksudi ilitumika katika kuteua riwaya ya Paradiso na Kidagaa
Kimemwozea.Mbinu anuwai za kimaelezo zilitumika katika kuchambua data na kuwasilisha
matokeo kwa lugha ya nadhari kuambatana na malengo ya utafiti.Maarifa yaliyopatikana katika
utafiti huu yatakuwa na mchango mkubwa katika maarifa yaliyopo kuhusu vijana na masuala ya
dini katika jamii.Mapendekezo ya utafiti huu yatasaidia viongozi wa madhehebu tofauti katika
harakati za kujenga upya maadili yanayozidi kumomonyoka miongoni mwa vijana. Utafiti huu
utatumika na wasomi,waandishi na wataalamu wengine katika kutafitia masuala yanayohusiana
na dini.Isitoshe,utafiti huu utatumika kama hazina ya marejeleo ya siku za usoni.
Description
Keywords
Utafiti, Udhanaishi, malengo, Mihimili mikuu, marejeleo