Thesis:
Nafasi ya wahusika wazee katika riwaya teule za Kiswahili

Abstract

Utafiti huu ulichunguza nafasi ya wazee katika riwaya mbili za Kiswahili ambazo ni Mkamandume (Said A. Mohammed 2013) na Tumaini (Clara Momanyi 2006). Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni; Kutambua sifa za wahusika wazee katika riwaya teule, Kuchunguza mchango wa wahusika wazee katika kuendeleza maudhui katika riwaya za Mkamandume (2013) na Tumaini(2006), na kubainisha jinsi wahusika wazee wamefanikisha matumizi ya fani katika riwaya za Mkamandume (2013) na Tumaini (2006). Utafiti huu uliongozwa na nadharia mseto ambayo ni: uhalisia na umuundo katika kukusanya na kuhakiki data. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka kwenye riwaya mbili zilizoteuliwa. Utafiti huu ulikuwa wa kimaelezo ikiwa na maana kuwa ulichunguza sifa zinazobainika za jambo linalotafitiwa. Utafiti huu ulifanyika kwenye maktaba. Mtafiti alisoma vitabu viwili pamoja na makala mengine yaliyomsaidia kukidhi dhamira ya utafiti. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia njia ya uchambuzi wa kimaelezo. Kwa mujibu wa Adam (2014) hii ni mbinu ambayo humpa mtafiti idhini ya kusoma au kuisikiliza kazi ya fasihi, kutambua maudhui, mtazamo na falsafa ya kazi hii pamoja na mambo mengine muhimu. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kupitia maelezo baada ya kuchanganuliwa. Maelezo haya yalijikita katika ufafanuzi wa nafasi ya wahusika wazee katika riwaya zilizoteuliwa. Utafiti huu ulibaini kuwa wahusika wazee wametumika katika kukuza na kuendeleza maudhui mbalimbali, kuonyesha hulka za wahusika wazee na hatimaye kufanikisha matumizi ya fani mbalimbali katika riwaya zilizotafitiwa. Utafiti huu ni wa manufaa kwa wachanganuzi wa masuala ya kijamii yanayohusu wazee katika jamii, mashirika yasiyo ya kiserikali na ya kiserikali yanayoshughulikia wazee kupata uelewa zaidi kuhusu hali za wazee na nafasi yao katika jamii. Watafiti, wasomi na wahakiki wa fasihi watafaidika na utafiti huu kwa kuwa unachangia kujaza mapengo katika utafiti hasa kuhusu wahusika wazee.

Cite this Publication
Andrew, B. K. (2024). Nafasi ya wahusika wazee katika riwaya teule za Kiswahili. Mount Kenya University. https://erepository.mku.ac.ke/handle/123456789/7654

Usage Statistics

Share this Publication

  • Total Views 1
  • Total Downloads 31

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Mount Kenya University