Thesis:
Usawiri wa mandhari katika riwaya ya kiswahili: mfano wa kiu na kidagaa kimemwozea

dc.contributor.advisorDkt. Stanley Adika Kevogo
dc.contributor.authorWyckliffe Collins Jaoko
dc.date.accessioned2025-09-26T05:51:21Z
dc.date.graduated2025
dc.date.issued2025-05
dc.description.abstractMandhari hufasiliwa kuwa ni mahali na wakati ambapo kadhia, visa au matukio ya kifasihi hutendeka kwenye tungo zinazohusika. Madhari yanaweza kuwa halisi au hata ya kufikirika. Azma kuu ya huu utafiti ilikuwa kuchunguza usawiri wa mandhari katika riwaya ya Kiswahili tukiangazia riwaya ya Mohamed S. Mohamed, Kiu pamoja na ile ya Ken Walibora, Kidagaa Kimwemwozea. Utafiti ulinuiwa kuyaafikia malengo muhsusi yafuatayo: kubainisha aina za mandhari yaliyotumiwa kuwasilisha ujumbe katika riwaya ya Kiu na Kidagaa Kimemwozea, kutathmini mchango wa mandhari katika ujenzi wa sifa za wahusika katika riwaya ya Kiu na Kidagaa Kimemwozea, pamoja na kueleza mandhari yalivyochangia uendelezaji wa ploti ya hadithi katika Kiu na Kidagaa kimemwozea. Utafiti uliongozwa na mseto wa nadharia mbili – Uhalisia na Umuundo. Nadharia ya Uhalisia ilichangia katika kuangazia jamii jinsi ilivyo kwa ukamilifu wake nayo nadharia ya Umuundo ilichangia katika kusisitiza vipengele vya kazi ya sanaa kama vile msuko, uumbaji wa wahusika, mandhari na matumizi ya lugha. Aidha, ilibainisha uhusiano wa vipengele hivi katika kuikamilisha kazi ya kifasihi. Utafiti huu wa mkabala wa kithamano ulifanywa maktabani kwa kuzingatia muundo wa kiuchanganuzi. Eneo la utafiti huu lilikuwa ni fasihi andishi, hususan utanzu wa riwaya ya Kiswahili. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa ni riwaya 10 za kiuhalisia ambazo zinasawiri mandhari halisi. Sampuli ya riwaya mbili, Kiu na Kidagaa Kimemwozea, iliteuliwa kwa usampulishaji dhaminifu. Huu ni usampulishaji sinasibu ambapo sampuli huteuliwa kwa kuakisi sifa za kipekee zinazohitajika kwenye utafiti. Riwaya mbili zinazohusika ziliteuliwa kwa misingi ya wingi wa vifani vilivyochunguzwa, yaani usawiri wa mandhari. Pamoja na kuakisi malengo ya utafiti, utunzi wa riwaya teule uliambatana na mihimili ya mseto wa nadharia zilizoongoza utafiti. Data za utafiti zilikusanywa kwa njia ya usomaji makini. Huu ni usomaji wa kina wa matini kwa lengo la kupata uelewa wa ndani kuhusu matini inayosomwa na kuhakikiwa. Usomaji makini ulifanyika maktabani ambapo riwaya teule, vitabu, tasnifu na makala anuwai mkondoni zilihakikiwa. Data zilizokusanywa ziliainishwa kwa mujibu wa mihimili ya nadharia na malengo ya utafiti. Hatimaye, data ilichanganuliwa kwa mujibu wa yaliyomo na matokeo kuwasilishwa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kwamba mandhari yana mchango wa moja kwa moja katika kuwasilisha ujumbe anuwai katika riwaya teule. Mandhari yana mchango katika kujenga sifa za wahusika na pia katika ukuzaji wa ploti za riwaya teule. Matokeo ya utafiti huu yana tija kwa taasisi za ukuzaji mitaala. Yatawasaidia kuweka mojawapo ya vigezo vitakavyoongoza uteuzi wa vitabu vya fasihi kwa ngazi mbalimbali. Mandhari yatatumika kama kigezo mojawapo katika maamuzi ya uteuzi. Vile vile, matokeo ya uchunguzi yatakuwa na faida kwa wanariwaya na waandishi wa kazi za kifasihi kwa jumla. Yatawasaidia kutunga visa vinavyosawiri na kuakisi mandhari kuntu. Isitoshe, wahakiki wa kazi za fasihi watawezeshwa kubaini, kutathmini na kuchanganua mandhari anuwai pamoja na dhima zao katika kazi za kifasihi.
dc.identifier.urihttps://erepository.mku.ac.ke/handle/123456789/7284
dc.language.isosw
dc.publisherMount Kenya University
dc.subjectRiwaya
dc.titleUsawiri wa mandhari katika riwaya ya kiswahili: mfano wa kiu na kidagaa kimemwozea
dspace.entity.typeThesisen

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
TASNIFU FINAL PROJECT.pdf
Size:
3.4 MB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: