Maendeleo ya Kiswahili awali yalidhihirika kupitia kwa nyanja za biashara, siasa, dini na
baadaye elimu. Kwa sasa nchini Kenya elimu inachangia pakubwa katika ueneaji wa Kiswahili
kwa kuwa Kiswahili kinafunzwa kama somo na ni lugha mojawapo kati ya lugha rasmi nchini
Kenya.