Fasihi ya watoto ni fasihi ambayo walengwa wake wakuu ni watoto. Fasihi hii ina umuhimu
katika jamii kwa sababu ina dhima mbalimbali. Pamoja na umuhimu wa fasihi ya watoto
katika jamii, fasihi hii ilichelewa kutambuliwa katika nchi za Afrika na duniani kwa ujumla
ikilinganishwa na fasihi nyingine. Matokeo yake ni kwamba, fasihi hii imekuwa nyuma sana
katika nyanja mbalimbali hasa za kiutafiti na kiufundishaji.